• HABARI MPYA

    Tuesday, March 20, 2012

    PATA MISTARI YA NDOA YA MATESO YA JABALI LA MUZIKI MARIJAN RAJAB


    MARIJAN:-UBETI 1:-
    Niulizieni enyi walimwenguu..
    Huyu mwanaume anavyonitesaaa…
    Hii ndio haki au ni matesoo..
    Hii ndio haki au ni matesoooo…..

    UBETI 2: -
    Kanitoa kwetu kwa baba na mamaaa..
    kwa vigelegele na heshima nyingi..
    Tizameni sasa anavyonigeukaa..
    Tizameni sasa anavyonigeukiaa..
    Tizameni sasa anavyonigeukaaa.

    UBETI 3:-
    Ananipa mateso huku ugenini..
    sina hata ndugu wa kunisaidiaaa..
    Nami nina watoto jamani tabu gani..
    Nami nina watoto jamani tabu ganiii…,

    UBETI 4:
    Kwani kuolewa ni jambo la ajabu..
    Au kuolewaaa sawa na utumwaaa.
    Kama ndivyo hivyo mimi nimeshindwaa..
    kama ndivyo hivyo mimi nimeshindwaaaa….,

    UBETI 5:
    Natoa ushahidi kwako weee Mjumbee…
    Mwambie huyo bwana anipe talaka yangu..
    Nisije kuondokaa ikawa ni maneno oooh!
    Nisije kuondoka ikawa ni manenoo ooh!

    WAITIKIAJI: MARJANI, TOSILI NA RAJABU:-
    Mambo anayoyafanyaa..
    Ni aibu kusemaaa..
    Kwa kuwa leo nina uchungu
    Nitakuelezaaa aah!
    Hapa unapotuonaa..
    Hakuna chochote nyumbanii..
    Mume wangu haonekanii…
    sijui yuko wapii……

    Anababaishwa na anasa za mjini..
    Mimi kanitupa na watoto hawajali..
    Pesa zake zotee..
    zinaishiaa njee.
    Kwa makuku ya kukaangaa….
    Mimi na mkate mkavu..
    Nimechokaa mimii..
    Na mwanaume mlevi..
    Heri anipe talaka..
    Nirudi kwetu..
    Sikuzaliwa juu ya miti….
    Ninako kwetuu..
    Ninako kwetuuuu..
    Kwa baba na mama…aah!

    KIBWAGIZO:
    MARIJANI, TOSILI NA RAJABU:-
    Matesooo… Matesooo… matesoooooo….
    Yamezidi Nachokaaa

    MARJAN:
    Polee mamaaa aah!,
    Kwa tabu uliozipata..
    Lakini kwanza usichukuee..
    hatua hiyo mamaa…

    KIBWAGIZO:-
    MARJANI:
    Mimi na wazazi wake…
    tutamwita tumkanyeee..
    Akirudia mimi nitakuwaa..
    Shahidi yako mamaaa..

    KIBWAGIZO:-
    MARIJANI:
    Naona vibaya..
    Mmeishazaa watotooo..
    Mkitengana mtawapaa..
    Tabu watoto wenu mamaaa..aah

    KIBWAGIZO:
    Matesoo{Mamaa.aah!}
    Matesooo {Maa-aaa-aah!}
    Mateso matesoooo
    yamezidi nachokaaa…

    SEBENE
    KIBWAGIZO:
     RAJABU, MARIJANI NA TOSILI:
    Matesooo matesooo matesooo yamezidi nachokaaa
    Matesooo.. matesooo.. matesooo…
    yamezidi Nachokaaa aa..
    Matesooo.. Matesooo Matesoooo
    Yamezidi Nachokaaaaa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PATA MISTARI YA NDOA YA MATESO YA JABALI LA MUZIKI MARIJAN RAJAB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top