• HABARI MPYA

  Wednesday, June 06, 2018

  ZFA YAZIDI KUWAKA MOTO, RAIS NAYE ANG'ATUKA MCHANA KWEUPE

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  RAIS wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) Ravia Idarous Faina ameandika barua rasmi ya kujiuzulu nafasi yake.
  Ravia sasa ataungana na Makamu wa Rais wa ZFA Unguja, Mzee Zam Ali na Mkurugenzi wa ufundi Abdulghan Msoma ambao walitangaza kujiuzulu mwishoni mwa mwezi Mei, 2018.
  Katibu mkuu wa ZFA, Mohammed Ali Hilali (Tedy) amethibitisha kupokea barua hiyo ya Ravia.
  “Ni kweli ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake, barua ameileta leo Jumatano saa 9 za mchana”. Alisema Tedy.
  Ravia alipokea kijiti hicho cha Urais kutoka kwa Amani Makungu Juni mwaka 2013.
  Ravia Idarous (kulia) amejiuzulu Urais wa ZFA akiwafuata Makamu wake wa Unguja, Mzee Zam Ali na Mkurugenzi wa Ufundi, Abdulghan Msoma 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZFA YAZIDI KUWAKA MOTO, RAIS NAYE ANG'ATUKA MCHANA KWEUPE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top