• HABARI MPYA

  Sunday, June 10, 2018

  TYSON FURY ARUDI KWA KISHINDO AMPIGA MTU HADI AKIMBIA ULINGONI

  Bondia Sefer Seferi wa Albania akiwa amemshika miguu mpinzani wake, Muingereza Tyson Fury kumpunguza kasi baada ya kuelemewa na kipigo katika pambano lisilo la ubingwa la uzito wa juu usiku wa jana ukumbi wa Manchester Arena, zamani M.E.N Arena mjini Manchester. Seferi aligoma kuendelea na pambano raundi ya nne akibaki kwenye kona yake baada ya raundi ya tatu na Fury aliyekuwa anapigana kwa mara ya kwanza tangu Februari mwaka 2015 alipofungiwa kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu zilizopigwa marufuku michezoni akashinda kwa Technical Knockout (TKO) 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TYSON FURY ARUDI KWA KISHINDO AMPIGA MTU HADI AKIMBIA ULINGONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top