• HABARI MPYA

  Sunday, June 10, 2018

  SINGIDA UNITED YAMALIZA NAFASI YA TATU SPORTPESA SUPER CUP

  Na Mwandishi Wetu, NAKURU
  TIMU ya Singida United imemaliza katika nafasi ya tatu kwenye michuano ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa penalty 4-1 baada ya sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji, Kakamega Homeboyz Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Kenya.
  Kwa mara nyingine, kipa Peter Manyika Junior ameibuka shujaa wa Singida United baada ya kuokoa penalti moja ya Kakamega, huku nyingine mbili zikiota mbawa. 
  Na waliofunga penalti za Singida United ni Miraji Adam, Shafiq Batambuze, Danny Lyanga na winga Deus Kaseke aliyechaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi, huku klabu yake ikizawadiwa kitita cha dola za Kimarekani 7, 500 na Kakamega wakipewa dola 5,000. 

  Kwa mara nyingine, kipa Peter Manyika Junior ameibuka shujaa wa Singida United

  Katika dakika 90 za mchezo huo, Wicklif Opondo alifunga bao la Kakamega na Danny Lyanga akawafungia Singida United.
  Bingwa wa SportPesa Super Cup atapata dola za Kimarekani 30,000 pamoja na nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, England. 
  Fainali ya SportPesa Super Cup inaendelea hivi sasa Uwanja wa Afraha na mshindi wa pili atajipatia dola za Kimarekani 10,000, wakati timu nyingine zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500. 
  Gor Mahia ndiye bingwa mtetezi ambaye mwaka jana iliifunga AFC Leopards 2-1 katika fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kila la heri Simba SC. Tunataka kupokea Kombe Dar es Salaam kesho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED YAMALIZA NAFASI YA TATU SPORTPESA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top