• HABARI MPYA

    Wednesday, June 13, 2018

    SALAH AFANYIWA VIPIMO VYA BEGA KAMA YUKO TAYARI KUCHEZA KOMBE LA DUNIA


    Mohamed Salah anapambana ili kuwa fiti aweze kuichezea Misri kuanzia mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    RATIBA YA MISRI KOMBE LA DUNIA

    Juni 15: Uruguay - Ekaterinburg - Saa 1 usiku
    Juni 19: Urusi - St Petersburg - Saa 7 usiku
    Juni 25: Saudi Arabia - Volgograd - Saa 9 Alasiri
    WINGA Mohamed Salah anapambana ili kuwa fiti aweze kuichezea Misri kuanzia mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia  nchini Urusi na jana amefanyiwa vipimo vya bega lake.
    Nyota huyo wa Liverpool ushiriki wake wa Urusi upo shakani baada ya kulazimika kutoka nje kipindi cha kwanza kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zaidi ya wiki mbili zilizopita.
    Hiyo ni baada ya kuumizwa bega la kushoto na Nahodha wa Real Madrid, Real Madridkatika mchezo ambao timu yake ilichapwa mabao 3-1.
    Chama cha Soka Misri (EFA) bado kina matumaini atacheza kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Uruguay mjini Ekaterinburg, lakini kimesema ni mapema kuthibitisha. 
    "Anaendelea kuimarika vizuri. Pamoja na hayo, siwezi kuthibitisha leo kwamba atacheza katika mechi ya kwanza,' amesema Mkurugenzi Mtendaji, Ehab Lehita.
    "Ninachoweza kusema ni kwamba tunatumai atacheza mechi katika mechi hii,". 
    Bado hajafanya mazoezi na wenzake, lakini ameorodheshwa kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya fainali za kwanza za Kombe la Dunia kwa Misri ndani ya miaka 28.
    Aliibuka Uwanja wa Akhmat Arena mjini Grozny, ambako Misri wameweka kambi, kwa ajili ya mazoezi jana jioni lakini akaishia kufanyishwa mazoezi ya bega.
    Salah amepigwa picha akifanyiwa vipimo vya bega lake la kushoto juu ya uimara wake.
    Misri wanaanza kampeni yao ya kuwania Kombe la Dunia Ijumaa dhidi ya Uruguay kabla ya kumenyana na Urusi na Saudi Arabia katika mechi za Kundi A.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SALAH AFANYIWA VIPIMO VYA BEGA KAMA YUKO TAYARI KUCHEZA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top