• HABARI MPYA

  Friday, June 08, 2018

  OKWI, TSHISHIMBI, KUTINYU NA CHIRWA WABANANISHWA NA WAZAWA 11 TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MSIMU LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WACHEZAJI wa kigeni, Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu, Mzambia Obrey Chirwa, Papy Kabamba Tshishimbi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Waganda Shafiq Batambuze na Emmanuel Okwi ni miongoni mwa wachezaji wachezaji 15 walioteuliwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika sherehe zitakazofanyika Juni 23 mwaka huu.
  Kutinyu, Batambuze wa Singida United, Chirwa, Tshishimbi wa Yanga na Okwi wa Simba SC watachuana na wachezaji wengine 11 wazawa ambao ni Kelvin Yondani wa Yanga, Mudathir Yahya wa Singida United, Adam Salamba wa Lipuli, Habibu Kyombo wa Mbao FC, John Bocco, Shiza Kichuya na Erasto Nyoni wa Simba, Marcel Kaheza wa Maji Maji), Yahya Zaid wa Azam na Hassan Dilunga wa Mtibwa Sugar.

  Licha ya Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL, pia siku hiyo katika sherehe zitakazofanyika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam kutatolewa tuzo mbalimbali ikiwemo ya Bingwa wa VPL, Mshindi wa Pili, Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne na Mfungaji Bora. 
  Tuzo nyingine ni Timu yenye Nidhamu Bora, Mchezaji Bora wa Ligi ya Vijana (Tuzo ya Ismail Khalfan), Mchezaji Bora Chipukizi, Mwamuzi Msaidizi Bora, Mwamuzi Bora,Kipa Bora, Kocha Bora, Goli Bora, Kikosi Bora cha Msimu na Mchezaji wa Heshima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OKWI, TSHISHIMBI, KUTINYU NA CHIRWA WABANANISHWA NA WAZAWA 11 TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MSIMU LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top