• HABARI MPYA

  Friday, June 15, 2018

  ALLIANCE NA BIASHARA UNITED KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI JUMAPILI NYAMAGANA

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  TIMU ya Alliance FC Jumapili itakuwa na mchezo wa kirafiki na jirani zao kutoka Musoma mkoani Mara, Biashara United utakaofanyika Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
  Timu hizo za Kanda ya Ziwa, zote zitacheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao baada ya kupanda katika msimu uliopita wa Ligi Daraja la Kwanza. 
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Mwanza, Mkurugenzi wa Alliance FC shule ya Alliance, James Bwire amesema kwamba mchezo huo ni maalum kwa timu zote kuanza maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
  Bwire amesema amesema kwamba mchezo huo utakaowapa makocha wa timu zote taswira ya vikosi vyao wakati huu wa usajili, utaanza Saa 10:00 jioni. 

  Alliance FC watamenyana na Biashara United Jumapili Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza

  Msimu ujao, Mwanza itakuwa na timu mbili tena Ligi Kuu, pamoja na Alliance, nyingie ni Mbao FC iliyosalia baada ya msimu wake wa pili tangu ipande kufuatia kushuka kwa wakongwe, Toto Africans, wakati Biashara inarejea kwa jina jipya tangu ishuke kama Polisi Mara mwaka 2003 katika msimu ambao ilipanda.
  Pamoja na Biashara na Alliance, timu nyingine zilizopanda Ligi Kuu msimu huu ni Coastal Union ya Tanga, Manispaa ya Kinondoni (KMC), JKT Ruvu na African Lyon zote za Dar es Salaam – na baada ya kushuka kwa Maji Maji ya Songea na Njombe Mji FC, msimu ujao Ligi Kuu itakuwa na timu 20. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALLIANCE NA BIASHARA UNITED KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI JUMAPILI NYAMAGANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top