Nyota ya mchezo wa leo ilikuwa upande wa kiungo wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki aliyefunga mabao matatu pele yake, huku mengine yalifungwa na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele na winga Mghana, Bernard Morrison.
Aziz Ki alifunga bao la kwanza kwa penalti dakika ya 42 baada ya Mayele kuangushwa kwenye boksi, la pili kwa shuti la umbali wa mita 30 dakika ya 45 na ushei na la tano kwa penalti pia kufuatia Clement Mzize kuangushwa kwenye boksi pia dakika ya 90.
Mayele alifunga bao la tatu dakika ya 49 baada ya kuwatoka mabeki wa Kagera na kumchambua kipá Said Kipao na Morrison akafunga la nne kwa shuti la umbali wa mita 18 dakika ya 84.
Yanga sasa wanafikisha pointi 68 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi nane zaidi ya watani, Simba SC baada ya wote kucheza mechi 25, wakati Kagera Sugar wanabaki na pointi zao 32 za mechi 26 nafasi ya nane.
Mechi ijayo ni dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC Jumapili ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment