• HABARI MPYA

    Tuesday, April 11, 2023

    GEITA GOLD YAWAPIGA KMC 2-0 PALE PLE DAR


    TIMU ya Geita Gold imepata ushindi wa ugenini wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya Geita Gold leo yamefungwa na Elas Maguri dakika ya pili na Geoffrey Julius dakika ya 81 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 37 na kurejea nafasi ya tano, ikiizidi pointi mbili Namungo FC baada ya wote kucheza mechi 26.
    Kwa upande wao, KMC wanabaki na pointi zao 26 nafasi ya 14 baada ya wao pia kucheza mechi 26.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GEITA GOLD YAWAPIGA KMC 2-0 PALE PLE DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top