• HABARI MPYA

    Sunday, March 15, 2026

    SINGIDA BLACK STARS YAICHAPA MBEYA CITY 4-1 BABATI

    TIMU ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni hii Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara.
    Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na kiungo Mghana, Emmanuel Kwame Keyekeh dakika ya 31, winga Mrundi Mossi Nduwumwe dakika ya 69 na beki wa kushoto, Mghana pia, Ibrahim Imoro dakika ya 72 na 86, baada ya Vitalis Mayanga kuanza kuifungia Mbeya City dakika ya 14. 
    Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 22 katika mchezo wa 14 na kupanda kwa nafasi nne hadi ya sita, wakati Mbeya City inabaki na pointi zake 13 za mechi 16 sasa nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.    
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA BLACK STARS YAICHAPA MBEYA CITY 4-1 BABATI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top