• HABARI MPYA

  Tuesday, December 27, 2022

  SINGIDA BIG STARS YAWAPIGA DODOMA JIJI 1-0 PALE PALE JAMHURI

  BAO pekee la nyota Mbrazil, Bruno Gomes dakika ya 80 limeipa Singida Big Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa jana Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Kwa ushindi huo, Big Stars wanafikisha pointi 34, ingawa wanabaki nafasi ya nne wakizidiwa pointi tatu na Azam FC baada ya wote kucheza mechi 18, wanabaki Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 18 za mechi 18 nafasi ya 12.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA BIG STARS YAWAPIGA DODOMA JIJI 1-0 PALE PALE JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top