• HABARI MPYA

  Wednesday, December 21, 2022

  GEITA GOLD YATOA SARE 1-1 NA AZAM FC NYANKUMBU


  WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
  Ni wageni, Azam FC waliotangulia kwa bao la mshambuliaji wake Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 15, kabla ya kiungo Offen Francis Chikola kuisawazishia Geita Gold kwa penalti dakika ya 69.
  Kwa matokeo hayo, Geita Gold inafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya sita, wakati Azam FC sasa ina pointi 37, baada ya wote kucheza mechi 17, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa mabao na Simba SC ambayo ina mechi moja mkononi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YATOA SARE 1-1 NA AZAM FC NYANKUMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top