• HABARI MPYA

  Saturday, December 17, 2022

  SINGIDA STARS YAICHAPA PRISONS 2-1 PALE PALE SOKOINE

  TIMU ya Singida Big Stars imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Singida Big Stars yamefungwa na Bruno Gomes dakika ya tano na Meddie Kagere dakika ya 57, wakati la Tanzania Prisons limefungwa Jumanne Elfadhil kwa penalti dakika ya 79.
  Kwa ushindi huo, wanafikisha pointi 30 katika mchezo wa 16, ingawa wanabaki nafasi ya nne wakizidiwa pointi nne na vigogo, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA STARS YAICHAPA PRISONS 2-1 PALE PALE SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top