• HABARI MPYA

  Friday, December 02, 2022

  KAGERA SUGAR YAICHAPA IHEFU KIBOKO YA YANGA 2-0 KIRUMBA


  WENYEJI, Kagera Sugar wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Eric Mwijage dakika ya 67 na Hamisi  Kiiza dakika ya 83 Na kwa ushindi huo wanakamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza wakiwa na pointi 21 na kupanda  nafasi ya sita.
  Kwa upande wao, Ihefu SC baada ya kipigo cha leo wanakamilisha michezo yao 15 ya mzunguko wa kwanza wa Ligi kwa kuvuna pointi 11 tu wakiwa nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAICHAPA IHEFU KIBOKO YA YANGA 2-0 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top