• HABARI MPYA

  Wednesday, December 07, 2022

  YANGA SC YAIPIGA NAMUNGO FC 2-0 PALE PALE MAJALIWA


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wamekamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC usiku Uwanja wa leo Uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa mkaoni Lindi.
  Mabao ya Yanga leo yamefungwa na Wakongo yote, la kwanza kiungo na Mchezaji Bora wa msimu uliopita, Yanick Litombo Bangala dakika ya 40 na winga Tuisila Kisinda dakika ya 82.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC inamaliza mzunguko wa kwanza na pointi 38, ikiendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tatu zaidi ya Azam FC wanaofuatia baada ya wote kucheza mechi 15.
  Kwa upande wao, Namungo FC baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 18 za mechi 15 nafasi ya tisa kwenye ligi ya timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAIPIGA NAMUNGO FC 2-0 PALE PALE MAJALIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top