• HABARI MPYA

  Saturday, December 31, 2022

  MAN CITY YAAMBULIA SARE 1-1 KWA EVERTON


  MABINGWA watetezi, Manchester City wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Everton Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mshambuliaji Mnorway, Erling Haaland alianza kuifungia Man City dakika ya 24 hilo likiwa bao lake la 27 la msimu, kabla ya Demarai Gray kuisawazishia Everton dakika ya 64.
  Kwa matokeo hayo, Man City inafikisha pointi 36, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi saba na vinara, Arsenal baada ya wote kucheza mechi 16.
  Kwa upande wao, Everton wanabaki na pointi zao 15 za mechi 17 nafasi ya 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAAMBULIA SARE 1-1 KWA EVERTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top