• HABARI MPYA

  Friday, December 30, 2022

  10BET TANZANIA YATAJA WASHINDI WA PROMOSHENI YA KOMBE LA DUNIA


  KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya 10bet imetangaza wazawadia washindi mbalimbali 50 wa promosheni ya kombe la dunia (WC Bonanza Promotion).
  Michuano ya kombe la dunia ilifanyika nchini Qatar na timu ya Argentina chini ya nahodha wao, Lionel Messi ilitwaa ubingwa.
  Meneja Masoko wa kampuni10bet Tanzania George Abdulrahman alisema kuwa kati ya washindi hao 50, washindi 10 walizawadiwa simu janja (smartphones) ambapo washindi wengine 20 walizawadiwa jezi za timu za mataifa mbalimbali yaliyoshiriki katika michuano hiyo na washindi 30 walizawadiwa fedha taslimu.
  Washindi hao wamefanikiwa kushinda zawadi mbalimbali baada ya kufanikiwa kupata pointi nyingi kati ya maelfu ya mashabiki wa soka waliokuwa wakibashiri matokeo mbalimbali wakati wa michuano hiyo na tayari washindi hao  wamekwisha chukua zawadi zao.
   “Tunajisikia fahari kubwa kuwazawadia wmashabiki wa soka walioshiriki kwa kubashiri kupitia michezo  yetu mbalimbali,” alisema Mlay.
  Mlay pia aliwaomba mashabiki wa soka wenye umri kuanzia miaka 18 kuanza kubashiri na kampuni yao ili kushinda zawadi mbalimbali pamoja na fedha taslimu.
  “Tunawaomba mashabiki kuendelea kubashiri na kampuni yetu ambapo mbali ya fedha, wataweza kushindia zawadi mbalimbali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 10BET TANZANIA YATAJA WASHINDI WA PROMOSHENI YA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top