• HABARI MPYA

  Saturday, December 10, 2022

  AZAM FC YAITANDIKA MALIMAO 9-0 KOMBE LA TFF CHAMAZI


  TIMU ya Azam FC imefanikiwa kusonga mbele Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 9-0 dhidi ya Malimao FC ya Katavi jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC katika mchezo huo yamefungwa na Sospeter Bajana, Shaaban Iddi Chilunda, Keneth Muguna, Kipre Junior, Abdul Suleiman ‘Sopu’ mawili, Yahya Zayd, Cyprian Kachwele na David Chilawanga.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAITANDIKA MALIMAO 9-0 KOMBE LA TFF CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top