• HABARI MPYA

  Thursday, December 29, 2022

  MAN CITY YAWACHAPA LEEDS UNITED 3-1 ELLAND ROAD


  TIMU ya Manchester City jana imewatandika wenyeji, Leeds United mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Elland Road Jijini Leeds, West Yorkshire.
  Mabao ya Man City yamefungwa na Rodri dakika ya 45 na Erling Haaland mawili dakika ya 51 na 64, wakati la Leeds limefungwa na Pascal Struijk dakika ya 73.
  Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 35, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na Arsenal baada ya wote kucheza mechi 15, wakati Leeds United inabaki na pointi zake 15 za mechi 15 nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAWACHAPA LEEDS UNITED 3-1 ELLAND ROAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top