• HABARI MPYA

  Wednesday, December 21, 2022

  PRISONS YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 SOKOINE


  WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Zabona Khamis dakika ya tatu na Samson Mbangula dakika ya 78 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 18 katika mchezo wa 17 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 11.
  Kwa upande wao, Dodoma Jiji wanateremkia nafasi ya 12 wakizidiwa tu wastani wa mabao na Prisons baada ya wote kucheza mechi 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top