• HABARI MPYA

  Monday, December 26, 2022

  POLISI TANZANIA YATOA SARE 3-3 NA COASTAL MOSHI


  WENYEJI, Polisi Tanzania wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3 na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Mabao ya Polisi Tanzania yamefungwa na Ally Rutibinga dakika ya 10 na Kelvin Sabato dakika ya 41 na 80, wakati ya Coastal Union yamefungwa na Vincent Abubakar dakika ya 18, Chilo Mkama aliyejifunga dakika ya 48 na Gustapha Simon dakika ya 89.
  Kwa matokeo hayo kila timu ikicheza mechi ya 18 ya msimu, Polisi Tanzania wanafikisha pointi 10, ingawa wanaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 wakizidiwa pointi tano na Coastal Union inayobaki nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  1 comments:

  Item Reviewed: POLISI TANZANIA YATOA SARE 3-3 NA COASTAL MOSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top