• HABARI MPYA

  Saturday, December 17, 2022

  KAGERA SUGAR YATOA SARE 2-2 NA AZAM FC KAITABA


  WENYEJI, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya 2-2 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Yussuf Mhilu dakika ya 12 na Meshack Abraham dakika ya 62, wakati ya Azam FC yamefungwa na Iddi Suleiman’l ‘Nado’ dakika ya 68 na Mkongo, Idris Mbombo dakika ya 87.
  Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 36 katika mchezo wa 16, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao, Kagera Sugar wanabaki na pointi zao 22 za mechi 19 nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YATOA SARE 2-2 NA AZAM FC KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top