• HABARI MPYA

  Saturday, December 31, 2022

  AZAM FC YAMALIZA MWAKA NA USHINDI WA 6-1 DHIDI YA MBEYA CITY


  WENYEJI, Azam FC wamefunga mwaka kwa kishindo baada ya kuwatandika Mbeya City mabao 6-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ mawili dakika ya 22 na 54, Mzimbabwe Prince Dube dakika ya 51, Mkenya Kenneth Muguna dakika ya 56, Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 71 na Cleophace Mkandala dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 40, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi nne na Simba na 10 na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 19.
  Kwa Mbeya City ambayo bao lake pekee la limefungwa na Richardson Ng’ondya dakika ya 78 inabaki na pointi zake 21 za mechi 19 nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAMALIZA MWAKA NA USHINDI WA 6-1 DHIDI YA MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top