• HABARI MPYA

  Friday, December 30, 2022

  BOCCO NA NTIBANZOKIZA WAPIGA HAT TRICK SIMBA YAITANDIKA PRISONS 7-1


  WENYEJI, Simba SC wamefunga mwaka vizuri baada ya ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mshambuliaji na Nahodha, John Bocco amefunga mabao matatu dakika za 12, 46 na 62 wakati akichezea kwa mara ya kwanza timu yake mpya, kiungo Mrundi Saido Ntibanzokiza pia amefunga mabao matatu dakika za 60, 63 na lingine limewekwa nyavuni na Shomari Kapombe dakika ya 88.
  Ni ushindi unaoifanya Simba ifikishe pointi 44 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Yanga SC.
  Kwa Tanzania Prisons ambayo bao lake limefungwa na Jeremiah Juma dakika ya 29 baada ya kichapo kikali cha leo inabaki na pointi zake 21 za mechi 19 nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOCCO NA NTIBANZOKIZA WAPIGA HAT TRICK SIMBA YAITANDIKA PRISONS 7-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top