• HABARI MPYA

  Saturday, December 17, 2022

  YANGA SC YAITANDIKA POLISI 3-0 NA 'KUTANUA KIFUA' KILELENI

  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

  Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Jesus Moloko dakika ya 47, Fiston Kalala Mayele dakika ya 77 na Clement Mzize dakika ya 86.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 41 katika mchezo wa 16 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya Azam FC wanaofuatia, wakati Polisi inabaki na pointi zake tisa za mechi 16 nafasi ya 16.     
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAITANDIKA POLISI 3-0 NA 'KUTANUA KIFUA' KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top