• HABARI MPYA

  Sunday, December 04, 2022

  GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA MTIBWA SUGAR NYANKUMBU


  WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
  Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Saido Ntibanzokiza kwa penalti dakika ya 34 na Juma Luizio dakika ya 45 na ushei, wakati ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Onesmo Mayaya dakika ya 10 na George Wawa aliyejifunga dakika ya 90 na ushei.
  Kwa matokeo hayo, Prisons inafikisha pointi 22 katika mchezo wa 15, ingawa inabaki nafasi ya tano wakati Mtibwa Sugar sasa ina pointi 21 za mechi 15 nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA MTIBWA SUGAR NYANKUMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top