• HABARI MPYA

  Saturday, December 17, 2022

  IHEFU SC YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-0 CHAMAZI


  TIMU ya Ihefu SC imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Ihefu SC yamefungwa na Obrey Chirwa dakika ya 85 na Michael Aidan aliyejifunga dakika ya 90.
  Kwa matokeo hayo, Ihefu wanafikisha pointi 14 katika mchezo wa 16 na kusogea nafasi ya 14, wakati Ruvu inabaki nafasi ya 15 na pointi zake 11 za mechi 16 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU SC YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top