• HABARI MPYA

  Saturday, December 31, 2022

  YANGA YAMALIZA MWAKA KWA USHINDI WA 1-0 MANUNGU


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameuga mwaka 2022 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 26.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC wanafikisha pointi 50 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya watani, Simba baada ya wote kucheza mechi 19.
  Kwa upande wao, Mtibwa Sugar baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi zao 24 za mechi 19 nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAMALIZA MWAKA KWA USHINDI WA 1-0 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top