• HABARI MPYA

  Thursday, December 15, 2022

  BEN POL AJA KAZI MPYA HATARI INAITWA NYUMBANI


  MSANII nguli wa Muziki hapa nchini Behnam Paul maarufu kama Ben Pol ameachia kibao kipya kinachofahamika kama Nyumbani. Katika wimbo wa Nyumbani Ben Pol ambaye asili yake ni Dodoma ameeleza raha na uzuri wa kurejea Nyumbani huku akisifia maadili mazuri, mtindo wa maisha, vyakula n.k katika jamii zetu za kitanzania.
  “Kwangu mimi Nyumbani ni zaidi ya sehemu tu, Nyumbani ni mahali popote ambapo unahisi upendo na amani, unajihisi kupata sapoti, unasikilizwa, unaeleweka, unapokelewa katika hali zote bila kujali mafanikio yanayoonekana kwa macho.
  Nawakaribisha wadau wote wa Muziki wa Tanzania kufurahia wimbo huu ambao sasa unapatikana katika mitandao yote tukiendelea kujivunia tulikotoka, kujivunia utanzania wetu, u-Afrika wetu, utu wetu” - Ben Pol.
  Video ya Nyumbani imefanyika katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani chini ya utayarishaji wa kampuni ya Redshot.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEN POL AJA KAZI MPYA HATARI INAITWA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top