• HABARI MPYA

  Tuesday, December 20, 2022

  MAYELE APIGA MBILI YANGA YAICHAPA COASTAL UNION 3-0 DAR


  MSHAMBULIAJI Mkongo, Fiston Kalala Mayele amefunga mabao mawili kuiwezesha Yanga SC kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mayele alifunga mabao yake dakika ya 29 na 47 hivyo kufikisha mabao 13 jumla kwenye ligi msimu huu na kuendelea kuongoza kwa mabao matatu ya Mzambia wa Simba, Moses Phiri.
  Aliyekamilisha ushindi wa Yanga leo ni kiungo Mzanzibari, Fiesal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 66 na sasa mabingwa hao watetezi wanafikisha pointi 44 katika mchezo wa 17 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi saba zaidi ya watani, Simba SC wenye mechi moja mkononi.
  Hali si nzuri kwa Coastal Union, kwani baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 15 za mechi 17 nafasi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE APIGA MBILI YANGA YAICHAPA COASTAL UNION 3-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top