• HABARI MPYA

  Tuesday, December 06, 2022

  MOROCCO YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA


  TIMU ya Taifa ya Morocco imeandika historia kubwa ulimwenguni baada ya kuitoa Hispania na kutinga Robo Fainali ya Kombe la Dunia 2022 mchujo Qatar.
  Baada ya sare ya 0-0 ikicheza kwa kujilinda ndani ya dakika 120, Simba wa Atlasi walikwenda kushinda kwa penalti 3-0, shujaa akiwa na kipa Bono aliyeokoa penalti mbili za Sergio Busquets na Carlos Soler baada ya ile kwanza iliyopigwa na Pablo Sarabia kwenda nje.
  Waliofunga penalti za Morocco ni Abdelhamid Sabiri, Badr Benoun na Achraf Hakimi na sasa Morocco  itamenyana na mshindi kati ya Ureno na Uswisi zinazomenyana baadaye leo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOROCCO YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top