• HABARI MPYA

  Wednesday, December 07, 2022

  COASTAL UNION YAICHAPA SINGIDA BIG STARS 2-1 LITI


  TIMU ya Coastal Union ya Tanga imepata ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Mabao ya Coastal Union yamefungwa na kiungo Mrundi, Emery Nimubona dakika ya 29 na mshambuliaji Mcameroon, Vincent Abubakar dakika ya 49, wakati la Singida Big Stars limefungwa na Deus Kaseke kwa penalti dakika ya  90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Coastal Union inakamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 15 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 12, wakati Big Stars inabaki na pointi zake 27 za mechi 15 pia nafasi ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAICHAPA SINGIDA BIG STARS 2-1 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top