• HABARI MPYA

  Wednesday, December 28, 2022

  MAN UNITED YAIBAMIZA NOTTINGHAM FOREST 3-0 OLD TRAFFORD


  WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Man United yamefungwa na Marcus Rashford dakika ya 19, Anthony Martial dakika ya 22 na Fred dakika ya 87.
  Kwa ushindi huo kikosi cha kocha Mholanzi Erik ten Hag kinafakisha pointi 29 katika mchezo wa 15, ingawa kinabaki nafasi ya tano kikizidiwa pointi moja Tottenham Hotspur ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, wakati Nottingham Forest wanabaki na pointi zao 13 za mechi 16 nafasi ya 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAIBAMIZA NOTTINGHAM FOREST 3-0 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top