• HABARI MPYA

  Saturday, December 17, 2022

  MTIBWA SUGAR YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA NAMUNGO MANUNGU


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Omary Suleiman alianza kuifungia Mtibwa Sugar dakika ya 78, kabla ya Peteme Counou kuisawazishia Namungo FC dakika ya 90 na ushei.
  Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 16 ikisogea nafasi ya tano, wakati Namungo inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 16 nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA NAMUNGO MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top