• HABARI MPYA

  Sunday, December 18, 2022

  DODOMA JIJI YAWAPIGA MBEYA CITY 2-1 PALE PALE SOKOINE


  TIMU ya Dodoma Jiji FC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Dodoma Jiji FC leo yamefungwa na Christian Ziggah dakika ya 17 na Zidane Sereri dakika ya 70, wakati la Mbeya City limefungwa na Eliud Ambokile dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 16 na kusogea nafasi ya 11, wakati Mbeya City wanabaki na pointi zao 20 za mechi 16 nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YAWAPIGA MBEYA CITY 2-1 PALE PALE SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top