• HABARI MPYA

  Sunday, December 04, 2022

  YANGA YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA PRISONS 1-0


  BAO la Feisal Salum Abdallah dakika ya 90 limeipa Young Africans ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Fei Toto alifunga bao hilo akimalizia pasi nzuri ya kiungo mwenza, Farid Mussa Malik baada ya shambulizi lilioanzishwa na winga Mghana, Bernard Morrison upande wa kulia.
  Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 35 katika mchezo wa 14 na kurejea kileleni mwa Ligi ikiizidi pointi moja Simba SC ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, wakati Prisons inabaki na pointi zake 15 za mechi 15 nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA PRISONS 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top