• HABARI MPYA

  Wednesday, December 07, 2022

  SIMBA QUEENS NA YANGA PRINCESS ZOTE ZAPIGWA UFUNGUZI LIGI YA WANAWAKE


  LICHA ya kusajili wachezaji wengi wa kigeni, mabingwa watetezi, Simba Queens na washindi wa pili wa msimu uliopita, Yanga Princess wote wameanza vibaya Ligi ya Wanawake msimu huu baada ya kufungwa jana na leo.
  Simba Queens ilichapwa 2-1 na JKT Queens katika mchezo wa ufunguzi jana Uwanja wa Mo Simba Arena, wakati Yanga leo imepigwa 1-0 na Fountain Gate Princess Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya JKT Queens jana yalifungwa na Eto’o Mlenzi na Fatuma Swaleh, huku la Simba Queens lilifungwa na Nahodha wake, Opa Clement wakati leo bao pekee la Fountain Gate limefungwa na mshambuliaji Mkenya, Cynthia Musungu aliyesajiliwa kutoka Hispania.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS NA YANGA PRINCESS ZOTE ZAPIGWA UFUNGUZI LIGI YA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top