• HABARI MPYA

  Thursday, December 15, 2022

  UFARANSA YAIFUATA ARGENTINA FAINALI KOMBE LA DUNIA


  MABINGWA watetezi, Ufaransa wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Morocco jana Uwanja wa Al Bayt mjini Al Khor nchini Qatar.
  Mabao ya Ufaransa yalifungwa na Theo Hernández dakika ya tano tu ya mchezo huo na Randal Kolo Muani dakika ya 79 na kuzima ndoto za Morocco kuweka rekodi mbili kwa mpigo.
  Sasa Ufaransa itakutana na Argentina katika Fainali tamu mno Jumapili Uwanja wa Lusail Iconic mjini Lusail.
  Nayo Morocco iliyoweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya Afrika kufika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia itamenyana na Croatia Jumamosi Uwanja wa Khalifa International mjiji Al Rayyan kuwania nafasi ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UFARANSA YAIFUATA ARGENTINA FAINALI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top