• HABARI MPYA

  Saturday, December 31, 2022

  LIVERPOOL YAICHAPA LEICESTER CITY 2-1 ANFIELD


  TIMU ya Liverpool imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leicester City usiku wa Ijumaa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield.
  Liverpool ilinufaika na makosa ya beki wa kati wa Leicester, Wout Faes aliyejifunga mabao yote mawili dakika za 38 na 45 baada ya kiungo Kiernan Dewsbury-Hall kutangulia kuwafungia wageni dakika ya nne.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 28 katika mchezo wa 16, ingawa inabaki nafasi ya sita wakati Leicester City inabaki na pointi zake 17 za mechi 17 nafasi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA LEICESTER CITY 2-1 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top