• HABARI MPYA

  Thursday, December 01, 2022

  KMC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA MBEYA CITY UHURU


  WENYEJI, KMC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mbeya City FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mlinzi Ibrahim Ame alianza kuifungia KMC dakika ya 27, kabla ya mshambuliaji Richardson Ng’ondya kuisawazishia Mbeya City dakika ya 34.
  Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 16 nafasi ya 10 na Mbeya City pointi 20 nafasi ya saba baada ya wote kukamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa ligi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA MBEYA CITY UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top