• HABARI MPYA

  Monday, December 05, 2022

  AZAM FC YAICHAPA POLISI TANZANIA 1-0 NA KUREJEA NAFASI YA PILI

  \

  TIMU ya Azam FC imepata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. 
  Bao pekee la Azam FC katika mchezo huo limefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 15 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 35 na kurejea nafasi ya pili, ikizidiwa tu wastani wa mabao na mabingwa watetezi, Yanga ambao wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao, Polisi Tanzania ambao leo wameanza kucheza chini ya kocha mpya, Mkongo, Mwinyi Zahera wanabaki na pointi zao tisa za mechi 15 nafasi ya mwisho, 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA POLISI TANZANIA 1-0 NA KUREJEA NAFASI YA PILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top