• HABARI MPYA

  Saturday, December 31, 2022

  DODOMA JIJI YAWACHAPA KAGERA SUGAR 2-0

  WENYEJI, Dodoma Jiji FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa Ijumaa Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Collins Opare dakika ya 24 na Hassan Mwaterema dakika ya 66 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 21 katika mchezo wa 19, ingawa wanabaki nafasi ya 12, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake 24 za mechi 19 nafasi ya sita.
    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YAWACHAPA KAGERA SUGAR 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top