• HABARI MPYA

  Friday, December 23, 2022

  SIMBA QUEENS NA YANGA PRINCESS ZAGAWANA POINTI KWA SARE YA 1-1  TIMU za Simba Queens na Yanga Princess zimegawana pointi katika mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Bao la Simba katika mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji wake Mkenya, Vivian Aquino likiwa la kusawazisha baada ya Mnigeria, Chioma Wogu kuanza kuifungia Yanga Princess.
  Kwa matokeo hayo, timu zote zinafikisha pointi nne baada ya kucheza mechi tatu, zikiwa zimefungwa moja moja na kushinda moja moja mbali na sare ya jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS NA YANGA PRINCESS ZAGAWANA POINTI KWA SARE YA 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top