• HABARI MPYA

  Monday, December 26, 2022

  SIMBA SC YAICHAPA KMC 3-1 UWANJA WA CCM KIRUMBA

  VIGOGO, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KMC leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. 
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji na Nahodha John Bocco dakika ya 16, winga Mghana Augustine Okrah dakika ya 55 na beki Mkongo, Henock Inonga Baka 'Varane' dakika ya 73, wakati la KMC limefungwa na Sadallah Lipangile dakika ya 52.
  Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 41, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi sita na mabingwa watetezi, mahasimu wao, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 18.
  Kwa upande wao KMC baada ya matokeo ya leo wanabaki na pointi zao 22 za mechi 18 pia katika nafasi ya tisa.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA KMC 3-1 UWANJA WA CCM KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top