• HABARI MPYA

  Saturday, December 24, 2022

  IHEFU SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 3-1 MBARALI

  WENYEJI, Ihefu SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Highland Estate huko Mbarali mkoani Mbeya.
  Mabao ya Ihefu SC leo yamefungwa na wachezaji wa zamani wa Azam FC, kiungo Joseph Mahundi dakika ya 60 na 88 na mshambuliaji Obrey Chirwa dakika ya 74, wakati la Mtibwa Sugar limefungwa na Ismail Mhesa dakika ya 52.
  Kwa ushindi huo, Ihefu SC wanafikisha pointi 17 katika mchezo wa 18 na kusogea nafasi ya 13, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 24 za mechi 18 nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 3-1 MBARALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top