• HABARI MPYA

  Wednesday, December 21, 2022

  SIMBA SC YATOA SARE NA KAGERA SUGAR 1-1 KAITABA


  WENYEJI, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Ni Kagera Sugar ya kocha Mecky Mexime iliyotangulia kwa bao la Deus Bukenya dakika ya 15, kabla ya beki Mkongo, Henock Inonga Baka kuisawazishia Simba dakika ya 38.
  Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar wanafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya sita, wakati Simba inayofikisha pointi 38 inabaki nafasi ya pili baada ya wote kucheza mechi 17.
  Ni mabingwa watetezi, Yanga SC wanaoendelea kuongoza Ligi Kuu baada ya raundi 17, wakiwa na pointi zao 44, wakati Azam FC yenye pointi 37 ni ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATOA SARE NA KAGERA SUGAR 1-1 KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top