• HABARI MPYA

  Sunday, December 25, 2022

  KAGERA SUGAR YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA GEITA GOLD KAITABA

  WENYEJI, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya 2-2 na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mabao ya Kagera Sugar leo yamefungwa na Deus Bukenya dakika ya 32 na Anuary Jabir dakika ya 53, wakati ya Geita Gold yamefungwa na Geoffrey Manyasa dakika ya 41 na Daniel Lyanga dakika ya 88.
  Kwa matokeo hayo, timu zote zinafikisha pointi 24 katika mchezo wa 18, Kagera Sugar ikienda nafasi ya sita na Geita Gold nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA GEITA GOLD KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top