• HABARI MPYA

  Sunday, December 11, 2022

  UFARANSA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA, YAITOA ENGLAND


  TIMU ya Taifa ya Ufaransa imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya England usiku wa jana Uwanja wa Al Bayt mjini Al Khor nchini Qatar.
  Nahodha Harry Kane alikuwa na usiku mgumu baada ya kukosa penalti ambayo ingeipa bao la kusawazisha England mechi iishe 2-2.
  Mabao ya Ufaransa jana yalifungwa na Aurelien Tchouameni dakika ya 17 na Olivier Giroud dakika ya 78, wakati la England lilifungwa na Harry Kane kwa penalti pia dakika ya 54, kabla ya kukosa penalti nyingine dakika ya 84.
  sasa Ufaransa itakutana na Morocco Jumatano, wakati Nusu Fainali nyingine ni kati ya Argentina na Croatia Jumanne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UFARANSA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA, YAITOA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top