• HABARI MPYA

  Sunday, December 18, 2022

  SIMBA SC YAITANDIKA GEITA GOLD 5-0 KIRUMBA


  VIGOGO, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya wenyeji, Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji na Nahodha, John Bocco dakika ya 12 na viungo Mzambia Clatous Chama dakika ya 40, Msenegal Pape Ousmane Sakho mawili dakika ya 47 na 75 na Mtanzania mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kibu Dennis Prosper dakika ya 89.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 37 katika mchezo wa 16 na kurejea nafasi ya pili, ikiizidi pointi moja Azam FC baada ya wote kucheza mechi 16, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 22 za mechi 16 nafasi ya saba.
  Na wanaoongoza Ligi Kuu ni mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 41 za mechi 16 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAITANDIKA GEITA GOLD 5-0 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top