• HABARI MPYA

  Sunday, December 25, 2022

  PRISONS YAICHAPA MBEYA CITY 2-1 SOKOINE

  TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Mbeya City leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Prisons yamefungwa na Zabona Khamis dakika ya 27 na Samsons Mbangula dakika ya 47, wakati la Mbeya City limefungwa na Baraka Mwalubunju dakika ya 61.
  Kwa ushindi huo, Prisons wanafikisha pointi 21 sawa na Mbeya City baada ya wote kucheza mechi18, ingawa Maafande wa Jeshi la Magereza wanabaki nafasi ya 11 wakizidiwa wastani wa mabao na mahasimu wao hao wa mji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAICHAPA MBEYA CITY 2-1 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top